Simba damu fans Simba damu fans Author
Title: SIMBA WAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI
Author: Simba damu fans
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya soka ya Simba sc imeanza vyema michuano ya mapinduzi baada ya kuifunga timu ya soka ya Jan...
Timu ya soka ya Simba sc imeanza vyema michuano ya mapinduzi baada ya kuifunga timu ya soka ya Jangombe Taifa kwa magoli 2-1 katika mchezo wa kombe la mapinduzi uliochezwa katika uwanja wa Amani.

Mpaka mapumziko Simba ilikuwa inaongoza kwa magoli 2-0 yaliofungwa na Mzamiru Yasin katika dakika ya 27 na Juma luizio katika dakika ya 43. Katika kipindi cha pili  wenyeji Jangombe walipata goli la kufutia machozi baada ya beki wa Simba Novaty lufunga kujifunga nakufanya matokeo yawe 2-1.

Mchezo wa mapema ulishuhudia Mabingwa watetezi Ura wakiifunga Kvz mabao 2-0.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top